Staa wa Hip-Hipo nchini, Nay wa Mitego amesema kwasasa anawaachia wanasheria wake kuhusu suala la nyimbo yake mpya “Pale Kati Patamu” kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kutokana na kukosa maadili katika jamii.

Nay amesema ana nyimwa uhuru wa kiuandishi kwa sababu hadi sasa nyimbo zake tatu zimeshafungiwa na BASATA kwasababu ya kukosa maadili kama anavyoambiwa na chombo hicho kinachoshughulikia masuala ya sanaa nchini.

BASATA imemuandikia barua staa huyo kwa ajiri ya kuhudhuria kikao kitakachojadili sababu ya kufungiwa kwa nyimbo hiyo “Pale Kati Patamu” ambayo aliiachia wiki iliyopita katika vituo mbali mbali vya radio nchini.

Nay amekumbwa na kifungo hicho cha kufungiwa nyimbo yake kutoka BASATA baada ya kutumia maneno yasiyofaa kwenye mistari ya wimbo huo mpya “Pale Kati Patamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *