Mwanamuziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amesema kuwa atayafanyia kazi maoni ya Rais Magufuli kuhusu kuboresha wimbo wake kwa namna ya pekee.

Nay wa Mitego amesema kuwa ataufanyia marekebisho wimbo huo lakini atahakikisha havuki mipaka kwenye marekebisho hayo.

Pia Nay amewataka wananchi na vyombo vya habari kuendelea kuzungumza ukweli na kutoa maoni yao lakini wasivuke mipaka iliyowekwa na nchi.

Nay alikamatwa wiki iliyopita kwa tuhuma za kusambaza wimbo wake wa ‘Wapo’ ambao Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) liliweka wazi kuwa haufai na una lugha za matusi.

Baada ya kukamatwa rapa huyo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alisema kuwa amezungumza na Rais Magufuli na rais akakiri kuupenda wimbo huo na akaagiza msanii huyo aachiwe huru na pia auboreshe wimbo huo  kwa kuongeza mambo mengine bila kupunguza alichokiimba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *