Wanamuziki wa kundi la Navy Kenzo, Aika na Nahreel wamesema lengo la kundi lao kwa sasa ni kwenda kwenye chart kubwa za muziki duniani Billboard pamoja na kwenye tuzo za Grammy.

Nany Kenzo limechaguliwa kuwania tuzo za MTV Africa Music Awards ambazo zitafanyika katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini ifikapo Oktoba 22 mwaka huu.

Navy Kenzo wamesema tayari kwa sasa wanakolabo za kutosha na wasanii wa Afrika ambazo zitawatangaza vizuri Afrika.

Kundi hilo mpaka sasa lina kolabo na Patoranking pamoja na Bana Boy wa Nigeria ambazo hazijatoka mpaka sasa.

Navy Kenzo ni kundi lililojizolea umaarufu nchini pamoja na nje ya nchi kutokana na ngoma zao kuwabamba mashabiki wao mpaka kupelekea kuwemo katika kinyang’anyiro cha tuzo za MTV MAMA zitakazofanyika mwezi huu nchini Afrika Kusni.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *