Baada ya Navy Kenzo kuachia albam yao mpya ‘Above In Minute’ mwishoni mwaka jana kundi hilo limeamua kuipeleka albam hiyo kimataifa zaidi baada ya kutoa ratiba ya ziara yao katika nchi mbali mbali.

Kundi hilo ambalo linaundwa na wasanii wawili ambao ni wapenzi Aika na Nahreel wametoa ratiba ya ziara yao ambayo itakuwa kwa ajili ya kuitangaza albam yao kimataifa zaidi ambapo watazunguka katika baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani pamoja na Bara la Asia.

Ziara hiyo intarajia kuanza tarehe 16 mwezi huu katika nchi ya Israel wakingozana na DJ D-Ommy ambaye ndiyo watamtumia kwenye ziara hiyo.

Baada ya hapo itafuata ziara ya Australia ambapo itakuwa mwezi Machi pamoja na mwezi April wakifuatiwa na nchi ya Congo na Rwanda mnamo mwezi Mei na Julai mwaka huu.

kenzo

Mwezi Agosti na Oktoba watakuwa katika nchi ya UK pamoja na Bara la Ulaya kwa ujumla huku mwezi Novemba na Disemba wakimalizia nchini Marekani.

Kupitia ukurasa wao ya Instagram, Navy Kenzo wameposti ratiba ya ziara yao ya kuipeleka Album hiyo Duniani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *