Navy Kenzo wamesema kuwa  ameshindwa kuachia kwa wakati kolabo yao na AliKiba kutokana na muimbaji huyo huyo kuwa busy mpaka kushindawa kuachia video.

Wasanii wanaounda kundi hilo Aika na Nahrel wamesema zaidi ya mara mbili walipanga kushoot video hiyo lakini wameshindwa kumpata msanii huyo kutokana na ubize pindi wanapomuhitaji.

Aika amesema kuwa kolabo na Alikiba ipo tayari kabisa lakini time table mkali wa ‘Aje’ imekuwa ngumu kwasasa.

Pia ameongeza kwa kusema mara ya pili wamepanga kushoot video lakini imeshindikana na wanataka kuachia nyimbo pamoja na video.

Kwa upande wake Nahreel amesema maara ya pili hii wamepanga kushoot video lakini yeye alikuwa yupo busy labda wakienda MTV MAMA kama wakipata muda wanaweza kufanya kwa sababu kila kitu kipo tayari kwenye nyimbo hiyo.

Navy Kenzo ni moja ya makundi maarufu na yanayofanya vizuri katika muziki wa Bongo fleva mpaka kupelekea kupata nafasi ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya MTV MAMA zitakazofanyika Afrika mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *