Kundi la muziki wa Bongo fleva nchini, Navy Kenzo wanatarajia kuzindua albam yao mpya itakayoitwa ‘Above In A Minute’ siku ya mkesha wa mwaka mpya Jumamosi December 31.

Nyimbo zilizomo kwenye album hiyo ni pamoja na Lini waliyomshirikisha Alikiba, Bajaj waliyomshirikisha msanii wa Nigeria, Patoranking, Done wakiwa na Mr Eazi, Morning, Bless Up wakiwa na msanii wao, Rosa Lee, Nipendelee wakiwa na kundi la Ghana, R2Bees.

Uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency Level 8 uliopo jijini Dar es Salaam.

kiba-navy

Wimbo wa kwanza kutoka kwenye album hiyo ni Feel Good waliyomshirikisha Wildad ambao ulitoka na video zake lakini nyingine bado hazijatoka.

Albam hiyo ni ya kwanza kwa kundi hilo toka kuanza kufanya kazi ya muziki baada ya wanamuziki wa kundi hilo Nahreel na Aika kujitoa kwenye kundi la Pah One miaka ya nyuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *