Navy Kenzo wanatarajia kuachia albam mpya ‘Above In a Minute’ ifikikapo mwezi Disemba mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nahreel amesema “THE WAIT IS OVER #Aim i cant wait for the world to listen to this Album #ComingOutThisDecember,”.

Kwenye albam hiyo Navy Kenzo wamewashirisha wasanii mbalimbali ndani na nje ya Tanzania ili kuleta radha tofauti ndani ya albam hiyo.

Vile vile kundi hilo lilidai kuwa watakuja na wimbo mkubwa zaidi kutoka kwenye album hiyo unaoweza kuwapeleka katika hatua kubwa zaidi kimuziki.

Kundi hilo linaundwa na wanamuziki wawili ambao ni Nahreel na Aika, wiki iliyopita walikuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki tuzo za MTV MAMA mwaka huu baada ya kuwemo kwenye kipengele cha ‘Best Group’ kwenye tuzo hizo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *