Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amefunguka na kusema maisha yake yapo hatarini na kudai kuwa watu ambao amewaanika kwenye sakata la ununuzi wa madiwani wanamtafuta.

Nassari amesema hayo ikiwa imepita siku moja toka alipokwenda kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupeleka ushahidi wake juu ya madiwani wa CHADEMA waliohama chama kwa kuhongwa rushwa na wateule wa Rais John Pombe Magufuli.

Kupitia akaunti yake ya Facebook ameandika “Maisha yangu yapo kwenye bonde la uvuli wa mauti, Maisha yangu yapo hatarini kwani Watesi wetu wananitafuta”.

Nassari, Godbless Lema pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa walikwenda kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kupeleka ushahidi wao juu ya sakata la kununuliwa kwa madiwani wa CHADEMA na kuhongwa fedha na ahadi mbalimbali kutoka kwa wateule wa Rais mkoani Arusha.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *