Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amsema kuwa Serikali isipokuwa makini wananchi hawatairudisha madarakani.

Nape Nnauye alisema hayo jana wakati akichangia katika bajeti ya Wizara ya Maji na kusema serikali inapaswa kufanya mambo kwa kuwafurahisha wananchi kwa kuwapa huduma bora na si vinginevyo.

Nape amesema serikali ilipoingia madarakani iliongeza mapato, kupunguza matumizi yasiayo ya lazima na tunaambiwa uchumi unakua kwa asilimia 7.2 lakini haya hayatakua na maana kama hayatatafsiriwa kwenye kuboresha huduma za jamii.

Amesema tunatakiwa tuone matokeo ya hatua hizi kwenye maboresho ya huduma za kijamii hasa maji la sivyo hazina maana.

Amesema bajeti iliyopita imetengwa bilioni 900 na bajeti hii bilioni 600 hapo watanzania hawawezi kuilewa na ukuaji wa uchumi hauwezi kubaki kwenye makaratasi

Amesema ilani ya CCM ndio mkataba kati ya CCM na wananchi na wasiposhughulikia kama walivyoahidi basi wananchi hawatawarudisha

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *