Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnuye amesema kuwa ataeleza ukweli wote siku ya Jumamosi hii jimboni kwake Mtama mkoani Lindi.

Nape ambaye aliondolewa kwenye nafasi ya waziri habari, Sanaaa, Utamaduni na Michezo wiki chache zilizopita baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi ya Saa 24 aliyoiunda kufuatia Kituo cha Clouds TV kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Nape aliahidi kupeleka ripoti hiyo kwa wakuu wake ambao ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais John Pombe Magufuli ambapo siku iliyofuata Rais aliteuliwa, Dkt. Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape.

Aidha Nape Nnauye alimshukuru Rais Magufuli kwa kumteua Mwakyembe kwenye nafasi hiyo na kuahidi kuendelea kuipa ushirikiano serikali.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nape ameandika;

“Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki. Narudi Mtama kuwaeleza wapiga kura wangu UKWELI WOTE. Ni Jmosi tar 8/4/17”–

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *