Sakata la utekaji limeendelea kung’ang’ania bungeni baada ya mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara kutaja majina ya wabunge watano akidai kuwa wamo katika orodha ya wanaotakiwa kutekwa na Idara ya Usalama wa Taifa.

Amesema hayo baada ya mbunge wa Nzega Mjini (CCM) Hussein Bashe kusema kuwa alitekwa na kuteswa na Idara ya Usalama wa Taifa baada ya mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe kutakiwa atoe uthibitisho kuwa Usalama wa Taifa ndiyo unahusika kuteka watu.

Akizungumza wakati akiomba mwongozo Bungeni jana, Waitara amesema kuwa kuna timu mbili za watu watatu zimeundwa na usalama wa Taifa kwa ajili ya kuteka watu.

Waitara alisema kuwa alipokea message kuhusu wabunge ambao ni target (Walengwa) wanaotakiwa kutekwa na Idara ya Usalama wa Taifa.

Mbunge huyo akawataja wabunge ambao wanatafutwa na Idara ya Usalama wa Taifa kuwa ni Nape Nnauye (Mtama-CCM), Hussein Bashe (Nzega Mjini-CCM), Godbless Lema (Arusha Mjini-Chadema), Peter Msigwa (Iringa Mjini-Chadema) na yeye mwenyewe.

Source: Mwananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *