Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amefunguka alichoambiwa na Tundu Lissu wakati wakitoka Bungeni kabla ya kupigwa risasi jana mjini Dodoma.

Nape amesema kuwa Lissu alimwambia maneno yafuatayo ‘Wewe Nape ni Mjomba wangu, kwanini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja mimi na wewe ni watuhumiwa hama CCM mjomba’.

Tundu Lissu alipigwa risasi jana na kupelekwa katika chumba cha upasuaji mkoani Dodoma kabla ya kusafirishwa kupelekwa Kenya katika Hospitali ya Aga Khan nchini humo.

Mbune wa Rombo, Joseph Selasini amesema kuwa Tundu Lissu alisafirishwa kwenda Kenya mida ya saa sita na nusu usiku na kusindikizwa na mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbiwe.

Wengine waliosafiri na Tundu Lissu ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa pamoja mke wa Tundu Lissu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *