Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amewaomba radhi viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini kwa lolote ambalo aliwakwaza wakati akitekeleza majukumu yake katika nafasi hiyo.

Nape amewaangukia wapinzani pamoja na makundi mengine ya watanzania ikiwemo viongozi wenzake ndani ya chama chake na nje ya chama.

Kiongozi huyo ameyasema hayo lleo wakati akikabidhi rasmi ofisi kwa kiongozi mpya anayechukua nafasi hiyo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey Polepole katika ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho Lumumba Jijini Dar es Salaam.

Nape pia amekiri kuwa chama hicho kimemsaidia zaidi kwenye maisha yake kuliko yeye alivyokisaidia wakati akiitumikia nafasi hiyo.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *