Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kuwa busara itumike katika zoezi la kutaja wasanii wanaotuhumiwa kuhusika na dawa za kulevya waliotajwa na Paul Makonda.

Kauli hiyo ameitoa jana Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sheria mpya wa huduma za habari.

Baadhi ya waliotajwa na kutakiwa kuripoti polisi kwa mahojiano ni pamoja na Vanessa Mdee, Wema Sepetu, Nyandu Toz, Chidi Benz, TID, Tunda na Babuu wa Kitaa.

 Nape amesema kuwa wizara yake inakiri kuwa tatizo hilo ni kubwa, na ilifikia hatua ya kuwasaidia baadhi ya wasanii kwenda kupata matibabu akiwemo msanii Ray C na kwamba wanaunga mkono jitihada zozote za kupambana na tatizo hilo.

Amesema tatizo lipo kwenye namna ya kuwaadhibu wanaogundulika kutumia dawa za kulevya, kwa maana ya sheria ipi itumike kuwashitaki, lakini pia tatizo lingine ni busara inayotumika kuwataja na kuwakamata watu ambao tayari wamekwisha athirika na dawa kulevya badala ya kuwasaidia.

Kwa mtazamo wake nape amesema hilo ni tatizo la jamii nzima, na kushauri jamii yote ya watanzania kushiriki katika kujenga maadili ya watoto.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *