Wananchi wa jimbo la Mtama mkoani Lindi wamemhoji mbunge wao, Nape Nnauye kuhusu ndege aina ya Bombardier, wakitaka kujua inawasaidiaje.

Ndege mbili aina ya Bombardier Dash 8 Q400 zilinunuliwa na Serikali kwa ajili ya kulifufua shirika la usafiri wa anga la Air Tanzania (ATCL), ambalo lilikuwa limezorota na kutishia uhai wake.

Ndege hizo zilizinduliwa na Rais John Magufuli Septemba 28, 2016 jijini Dar es Salaam.

Lakini wananchi wa Mtama bado hawajaona umuhimu wake na walimuhoji Nape, ambaye alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Jana Nape aliandika katika akaunti yake ya Twitter kuhusu utashi huo wa wananchi wake kuhusu Bombardier.

Kupitia akaunti yake ya twitter ameandika “Watu hawa wanapambana na hali zao! Waliniuliza bombardier ndiyo nini” na sie wa vijijini tutafaidikaje au ni kwenu mjini tu!?”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *