Aliyekuwa waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema kuwa yeye aliunda kamati ya kuchunguza kuvamiwa kwa Clouds Media na si kumchunguza RC.

Kupitia akaunti yake ya Twitter Nape ameandika “Niliunda Kamati Kuchunguza tukio la kuvamiwa kituo cha utangazaji siyo kumchunguza RC Kama RC alikuwa mmoja wa wavamizi, hayuko juu ya sheria.

Nape ambaye ni mbunge wa Mtama mkoani Lindi ameadnika maneno hayo baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusema kuwa waziri huyo alikuwa hana mamlaka ya kuunda kamati na kumchunguza mkuu wa mkoa.

Katika mahojiano na kituo cha Star Tv, Makonda amesema kuwa Nape hawezi kuunda kamati ya kumchunguza yeye kutokana vyeo vyao viko sawa kutokana na wote wanateuliwa na Rais wa nchi.

Kuhusu uvamizi wa Clouds Media Makonda amesema kuwa hakuvamia kituo hiko kama inavyoelezwa bali alikuwa ameenda kama anavyoendaka maeneo hayo.

Nape wakati alipokuwa waziri wa habari aliunda kamati ya kuchunguza tukio la uvamizi wa kituo cha Clouds Media lililofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *