Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ameruhusu uwanja wa Taifa kutumika tena katika mechi za vilabu vya soka pamoja na matukio ya kijamii kama ilivyokuwa zamani.
Kupitia taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari leo Januari 27 waziri Nape amesema kuwa wizara yake imeridhishwa na ukarabati uliofanywa katika uwanja wa taifa na hivyo ameruhusu tena uwanja huo kutumika.
Uwanja wa taifa ulifungiwa kutumiwa baada ya Simba kufanya uharibifu wa kutoka viti kwenye mechi ya ligi kuu iliyofanyika Oktoba 1 mwaka jana na kusababisha viti kuharibika.
Pia waziri Nape katika taarifa yake hiyo ametoa onyo kwa watumiaji wa uwanja huo kuwa waangalifu pindi wanapotumia ili kulinda miundombinu ya uwanja huo.