Aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amekabidhi ofisi ya wizara hiyo kwa Waziri wa mpya, Dkt. Harrison Mwakyembe.

Nape ambaye ni mbunge wa Mtama mkoani Lindi amekabidhi ofisi hiyo kwa Dkt. Mwakyembe mbele ya watumishi wa wizara hiyo mjini Dodoma.

Uteuzi wa Nape ulitenguliwa wiki iliyopita na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumuacha kwenye mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

mwak

Dkt. Mwakyembe ambaye alikuwa waziri wa Katiba na Sheria ambapo alihamishiwa kwenye wizara hiyo baada ya uwaziri wa katiba na Sheria kwenda kwa Profesa Palamagamba Kabudi.

Wakati wa makabidhiano hayo viongozi hao walionekana wakiwa kwenye furaha wakati wote wamakabidhiano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *