Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ameipongeza klabu ya Simba kwa kuomba radhi kufuatia mashabiki wake kuvunja viti zaidi ya 1700 katika uwanja wa Taifa na kuahidi kuvitengeneza

Nape ameonyesha kusikitishwa kwake juu ya utovu wa nidhamu uliooneshwa na mashabiki wa soka jambo ambalo limesababisha serikali kufungia timu za Simba na Yanga kucheza katika uwanja huo wa Taifa.

Pamoja na hayo Waziri Nape amesema serikali haikutaka kuunda kamati ya uchunguzi katika sakata hilo kwa madai kuwa kuunda kamati ni kupoteza pesa, raslimali na muda hasa kwa jambo ambalo lilionekana hadharani machoni pa watu wengi.

Aidha Waziri amesema asilimia 98 ya uwanja wa Uhuru umejengwa kwa saruji katika maeneo ya kukalia, hivyo mechi za Simba na Yanga ni ruksa kufanyika katika uwanja huo.

Baada ya tukio la mashabiki wa Simba kuvunja viti uwanjani, Msemaji wa Simba Haji Manara alijitokeza hadharani na kuomba radhi kwa watanzania kutokana na kadhia iliyosababishwa na mashabiki baada kutoridhia maamuzi ya mwamuzi Martin Saanya kuhusu goli lililofungwa na Amisi Tambwe.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *