Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye kupitia akaunti yake ya Twitter amesema kuwa ipo haja kama Taifa kuangalia vipaumbele vyetu.

Nape amesema kuwa anapokumbuka shida wanazozipata wananchi humfanya aonekane mkorofi kwa kuwa anasema ukweli.

kupitia ukurasa wake wa twitter huku akiambatanisha na picha ambayo inaonesha wananchi jinsi wanavyopata tabu kuvuka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili kwa kupita ndani ya maji hayo.

Nape ameandika kama ifuatavyo “Niliyashuhudia maisha haya mikoani kwa miezi 38, nadhani ndiyo nikiyakumbuka naonekana mkorofi !! iko haja kama Taifa kuangalia vipaumbele vyetu”.

Picha ya watu wakivuka kwenye mto iliyowekwa na Nape Nnauye kwenye akaunti yake ya Twitter.
Picha ya watu wakivuka kwenye mto iliyowekwa na Nape Nnauye kwenye akaunti yake ya Twitter.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *