Shirikisho la soka Barani Ulaya “UEFA” limetoa orodha ya wachezaji 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora Ulaya kwa msimu wa mwaka 2015/2016 ifikapo Agosti 25 mwaka huu.

Wachezaji watakaowania tuzo hiyo ni Gareth Bale – Real Madrid, Gian-luigi Buffon -Juventus , Antoine Griezmann – Atletico Madrid, Toni Kroos – Real Madrid , Lionel Messi -Barcelona.

Wengine ni Thomas Müller -Bayern Munich, Manuel Neuer – Bayern Munich , Laveran Ferreira (Pepe) – Real Madrid, Cristiano Ronaldo -Real Madrid na Luis Suarez –Barcelona.

Cristiano Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo baada ya kuisaidia klabu yake ya Real Madrid kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya, vile vile kuisaidia timu yake ya Taifa, Ureno kushinda kombe la mataifa ya Ulaya mwaka huu nchini Ufaransa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *