Umemis ‘ngoma mpya’ za WCB? Unataka collabo au unataka solo? Unataka ngoma mpya ya nani; Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Mavoko au Queen Darleen?

Kwa mujibu wa staa wa kundi hilo, Rayvanny, crew ya WCB inajipanga kuachia video ya collabo ya Queen Darleen na yeye, Rayvanny ya ngoma KIJUSO na baada ya hapo itakuwa zamu yake kuachia single nyingine.

Staa huyo ambaye ‘AMESHAPATA KIKI’ na sasa anafahamika kama mrithi wa Diamond Platnumz huku akitambulishwa kwenye majukwaa ya kimataifa na label hiyo amejinadi kuwa na ngoma nyingi zinazosubiri wakati ufike ili zitolewe.

Pamoja na Rayvanny kusema hayo lakini mashabiki pia wanatarajia staa mwingine wa lebo hiyo, Harmonize ataachia ngoma mpya hususani baada ya kuvunjika kwa uhusiano wake na staa wa Bongo Movie, Jacquiline Wolper.

Pamoja na hivyo lakini pia mashabiki hawajapata ngoma ya Diamond Platnumz akiwa peke yake kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *