Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka makubwa akilia upweke baada kuandika ujumbe kwenye ukurasa wa mchumba’ke, Billnass au Nenga akimtaka kurudi nyumbani haraka.

Billnass yupo Dubai ambapo inasemekana ameenda kwa shughuli za kibiashara ambazo mwanamuziki huyo anaendelea kufanya hivi karibuni.

Hivi karibuni Billnass alimvisha Nandy pete ya uchumba nyumbani kwao huku wakifichua kwamba ndoa rasmi haitapita mwezi wa sita.

Billnass alimjibu Nandy kwa kumueleza kuwa anatafuta vazi ambalo atavaa siku ya harusi ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wao.

“Nandy nakutafutia gauni la harusi, maana hizi vita zinanichanganya, tunaweza kufungia ndoa kwa kifaru,” anasema Billnas akimaanisha vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Nandy amekanusha madai kwamba amechepuka baada ya mtangazaji wa shirika la habari nchini humo, kumfumania usiku akisindikizwa kwenye gari na mwanamume mwingine ambaye Mwijaku alibaini si yule ambaye amemchumbia hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *