Aliyekuwa Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari ameitaka jamii kumthamini mtoto wa kike kwa kumpa haki zake zote kama anavyopewa mtoto wa kiume.

Mrembo huyo ameyasema hayo hayo wakati akipongeza kituo cha EATV kwa kuanzisha kampeni ya Namthamini kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike kupata pedi ili kuhudhuria masomo shuleni.

Akizungumza leo katika kilele cha kuazimisha siku ya mwanamke duniani mrembo huyo amesema pedi pekee yake haitoshi kumaliza au kutatua tatizo hilo kwa watoto wa kike bila ya kushirikishwa Wizara ya Elimu kwa lengo la utoaji elimu kwa jamii nzima ili watambue thamani ya mtoto wa kike.

 

Utafiti uliyofanywa na baadhi ya mashirika ya kutetea haki za mtoto wa kike zilibaini asilimia kubwa ya watoto wa kike wanashindwa kufanya vizuri masomo yao wakiwa shule kutokana na ukosefu wa pedi pindi wanapoingia hedhi.

Nancy Sumari ndiye Miss Tanzania pekee hadi sasa aliyeweka historia ya kuvaa taji la ‘Miss World Afrika’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *