Rais mpya wa Ghana, Nana Akuffo-Addo jana ameapisha rasmi kuchukua wadhifa huo baada ya kushinda uchaguzi uliopita nchini humo.

Maelfu ya wageni walialikwa kwenye sherehe katika Medani ya Uhuru mjini Accra nchini Ghana.

Akufo Addo, aliyewahi kuwa wakili wa haki za kibinaadamu, alimshinda aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, John Dramani Mahama, katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita.

Madaraka yamekabidhiwa kwa kiongozi Akufo-Addo kwa njia ya amani, jambo linaloonekana kuwa mfano mwema wa demokrasi barani Afrika ambako katika baadhi ya nchi, viongozi hawataki kun’gatuka

Baada ya kuapishwa kwa rais, sasa viongozi waliohudhuria sherehe hiyo, watajadili namna ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, anaondoka madarakani ambapo kiongozi huyo amekataa kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa mwezi Desemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *