Mwanamuziki wa Bongo fleva, Naj amesema kuwa afanyi kazi kwa kutafuta ‘kiki’ kwasababu anaamini ana kipaji cha hali ya juu kwa hiyo hawezi kufanya hivyo kama baadhi ya watu wanavyosema.

Naj amesema kwamba aoni kama kuna tatizo ila hayo mambo yanakuzwa na maneno ya watu ila kwa upande wake afanyi kazi kwa ‘kiki’, na kwa sasa chochote atakachokisema anaweza asieleweke hivyo ameamua ni bora akae kimya tu.

Kauli hiyo ya Naj inakuaja baada ya Mr. Brue¬† kutangaza kuchukua hatua za kisheria kwa Naj au Baraka endapo atagundua kuwa wao ndiyo walianzisha ile skendo iliyomuhusisha yeye kuwa anachepuka na Naj ili kuupa ‘kiki’ wimbo wao mpya.

Pia Blue amesema kuwa aliongea na Baraka na akasemea kuwa hajui uzushi huo umetokea wapi hivyo wakayamaliza bila ya kuwa na tatizo.

Hata hivyo Brue amesema kama hawa watoto wadogo ni wao ndiyo wameanzisha hii skendo  akigundua ni hivyo basi nitawachukulia hatua za kisheria.

Brue ameongea hivyo kutokana kwasasa ameoa na ana watoto wawili kwa hiyo hataki kugombana na mkewe kwasababu wametoka mbali.

Brue na Naj walikuwa wapenzi hapo nyuma kabla hawajatengana lakini kwasasa kila mtu ana ishu zake. Kwasasa Naj anatoka na mwanamuziki mwenzake wa Bongo fleva, Baraka Da Prince.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *