Mwanamke anayedaiwa kuwa jambazi sugu ameuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi jijini Nairobi nchini Kenya.

Kijana huyo ambaye ametambuliwa kama Claire Mwaniki aliuawa na polisi alfajiri na mapema jana katika mtaa wa kayole.

Taarifa zilizopo zinasema kuwa mwanamke huyo alikuwa na majambazi wengine wane wa kiume pale waliposhtukiwa na polisi wakitekeleza wizi katika eneo la Lower Chokaa, mtaa wa Kayole jijini Nairobi.

Anadaiwa kufyatulaina risasi na maafisa wa polisi akiwa na jambazi mwingine lakini wawili hao wakauawa.

Polisi waliwaandama baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wenzao kupitia WhatsApp kwamba majambazi hao walikuwa wamekwepa mtego waliokuwa wamewekewa.

Mkuu wa polisi wa mtaa wa Kayole Joseph Gichangi amesema kuwa  mwanamke huyo alikuwa mke wa mshukiwa wa ujambazi ambaye anafahamika vyema, ambaye bado anasakwa na polisi.

Alisema visa vya wanawake kujihusisha na magenge yanayotekeleza wizi wa kutumia mabavu vinaongezeka.

Mwanamke huyo anajitambulisha kama mwanafunzi wa zamani wa chuo kikuu cha Nairobi na mtu anayependa kufurahia maisha.

Mkuu wa polisi Nairobi Japheth Koome amesema magenge mengi ya wahalifu huwa na wanawake.

Aliongeza kuwa wakati mwingine hutumiwa na majambazi wa kiume kuwapelekea chakula mafichoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *