Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amekabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Naibu Waziri wizara hiyo Anastazia Wambura leo mjini Dodoma.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ofisi za wizara hiyo mjini Dodoma ambapo pia alikuwepo waziri wa wizara hiyo, Dkt Harrison Mwakyembe.

Naibu waziri Shonza ameteuliwa na Rais Magufuli kushika nafasi hiyo katika baraza jipya la mawaziri lililotangazwa wiki iliyopita.

Shonza anachukua nafasi ya Anastazia Wambura ambaye uteuzi wake umetenguliwa na Rais Magufuli katika baraza jipya la Mawaziri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *