Mwanamuziki na mtayarishaji wa Bongo fleva, Nahreel kutoka kundi la Navy Kenzo, ameeleza furaha yake juu ya kuanzishwa kwa EATV AWARDS na kusema kuwa ni heshima kubwa kwa wasanii.

Nahreel amesema tuzo hizo zitaleta heshima kubwa kwenye muziki wa Tanzania, kwani wao kama wasanii wanajivunia kuwa na tuzo za nyumbani.

Nahreel ameendelea kusema kuwa anatumaini tuzo hizo zitakuwa kubwa zaidi na kuja kubadilisha tasnia ya muziki wa Afrika Mashariki, kama zilivyo tuzo nyingine kubwa za kimataifa.

EATV AWARDS ndizo tuzo kubwa za kwanza kuanzishwa kwa nchi za Afrika Mashariki, na zitahusisha wasanii wa filamu na muziki wa nchi hizo moja kwa moja, zinazotarajiwa kufikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *