Mtayarishaji na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nahreel amefunguka na kusema kuwa hana mtoto wa nje na taarifa zinazosambaa amezaa na mwanamke mwingine ni uongo.

Katika hali inayoibua sintofahamu, Nahreel ameibuka na kukanusha tetesi kwamba ana mtoto nje ya uhusiano wake na Aika.

Nahreel ameandika; “Habari za mimi kuwa na mtoto nje zimekuwa ni nyingi na ni za uongo, naomba muheshimu familia yangu.

“Kutokana na habari zinazosambaa kwenye blogs mbalimbali na watu mbalimbali maarufu pia wamekuwa wakiposti bila kuwa na ushahidi wowote, hizi habari siyo za kweli.

“Nina watoto wawili Gold_navykenzo na Jamaika_navykenzo. Na nimezaa na mwanamke mmoja Aikanavykenzo Kuweni makini mnapotoa habari familia yetu haiendekezi umbeya ila hii imevuka mipaka.

Nahreel na Aika imekuwa ni kapo ya mfano kwa kuwa wamedumu kwa muda mrefu bila kokoro, lakini inavyoonekana kuna wanga wanataka kuharibu mambo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *