Muigizaji mkongwe wa vichekesho nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ amesema kuwa hawezi kuacha kuigiza kutokana na uigizaji upo kwenye damu kwa hiyo ataigiza mpaka atakapokufa.

Mzee Majuto mwaka jana aliwahi kutangaza kuacha uigizaji na kumrudia Mungu amefunguka na kusema kuwa ataendelea kuigiza mpaka anakufa kwa sababu uigizaji upo kwenye damu.

Muigizaji huyo amesema kuwa yeye hawezi kukubali kuona fani inachezewa chezewa na watoto hivyo ataendelea kuigiza mpaka siku atakayokufa kwa sababu uwezo wake ni wa hali ya juu kwenye kuandika na kuigiza.

Mzee Majuto akiwa na waigizaji wenzake kwenye moja ya filamu alizoigiza
Mzee Majuto akiwa na waigizaji wenzake kwenye moja ya filamu alizoigiza

Majuto amesema kuwa kuigiza kwake ni kama maradhi vile hivyo adhani kama anaweza kuacha na kukaa pembeni huku sanaa ikawa inachezewa na watoto wadogo kabisa.

Muigizaji huyo ni miongoni mwa waigizaji maarufu na waliojizolea umaarufu kutokana na fani hiyo ya uigizaji baada ya kugiza filamu kibao zilizojizoelea umaarufu kama vile Zima Ngoma, Inyee, na nyininge nyingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *