Muigizaji mkongwe wa Bongo Movie, King Majuto amewataka wasanii nchini ambao wapo katika tasnia hiyo kufanya kazi zenye ubora ili kufikia mafanikio yao.

Kauli ya muigizaji huyo inakuja kufuatia baadhi ya wasanii nchini kuwa na maisha ya kawaida licha ya kazi zao za sanaa kufika mbali.

Muigizaji huyu ambaye alitangaza kustaafu kuigiza amesema kuwa kwa sasa hivi wasanii wanapendwa na serikili inawatambua hivyo watumie fursa hiyo kufanya kazi.

Mzee Majuto amesema kuwa “Kwa hiyo msichoke, fanyeni jitihada, tengenezeni michezo yenye busara, tengenezeni michezo inayoeleweka msifanye ilimradi tu na heshimuni bodi ya filamu ili mfanye kazi nzuri”.

Soko la Bongo Movie kwasasa limeshuka kutokana na wasanii nchini kukosa ubunifu wa kutosha katika kazi zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *