Muigizaji wa filamu na mchekeshaji nchini Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ amefunguka na kusema kuwa mwaka 2017 amepanga kufanya mambo matatu ambayo yote anataka yaende pamoja.

Jambo la kwanza ni kuhusiana na sanaa yake ambapo amepanga kwa mwaka huu wa 2017 kuhakikisha kazi zake za sanaa anazisambaza mwenyewe na kuachana na wasambazaji wengine.

Mzee Majuto amesema jambo la pili katika mwaka huu ambalo pia atalifanya sana ni kuhakikisha ana mcha Mungu sana na jambo la mwisho ni kufanya kilimo na ufugaji ili kijiongezea kipato chake.

Muigizaji aliyeanza kuigiza miaka iliyopita na amefanikiwa sana kwenye sekta ya sanaa kutokana na kazi zake kuwabamba mashabiki wake wa ndani na nje ya nchi.

Mzee Majuto mwaka jana aliwahi kutangaza kuacha uigizaji na kumrudia Mungu amefunguka na kusema kuwa ataendelea kuigiza mpaka anakufa kwa sababu uigizaji upo kwenye damu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *