Muigizaji wa Tamthilia ya Siri za Familia, Haji Jumbe ambaye aliigizaji kama mzee Benson kwenye tamthilia hiyo inayorushwa na kituo cha runinga cha EATV anazikwa leo saa tisa alasili wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Muigizaji huyo amefariki jana jioni katika hospitali ya Kinondoni baada ya kusumbuliwa na maradhi ya tumbo.

Kabla ya kuigiza tamthilia ya Siri za Familia muigizaji huyo pia amewahi kuigiza matangazo yaliyokuwa yanaandaliwa na Dk Mwaka aliyekuwa anamiliki kituo cha tiba asilia cha Fore Plan Clinic kilichopo Ilala.

Tasnia ya filamu imekumbwa na msiba mkubwa kufuatia kifo cha muigizaji huyo aliyejizolea umaarufu kupitia uigizaji wake katika kazi za sanaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *