Muigizaji mkongwe wa vichekesho, Mzee Jangala amesema kuwa apendezwi na baadhi ya wasanii wa kiume wanaovaa nguo zinazobana, kutoboa masikio na kuonesha maumbile yao ambapo ni kinyume na maadili.

Mzee Jangala amesema vijana wanapaswa kujitambua na kuelewa maana ya utandawazi na siyo kuiga mambo mbalimbali ikiwemo kukaa uchi mbele za watu wazima kubadilisha maumbile yao halisi na kudai kuwa wanafuata utandawazi na kupotosha jamii zima.

Pia Mzee Jangala hakusita kuwasihi wasanii wa kizazi kipya kujitambua na kufanya mambo ya msingi katika jamii kwa kuwa wao ni watu ambao wana mashabiki ambao wanawaufatilia maisha yao na kuiga kila kinachofanywa na watu maarufu.

Muigizaji huyo aliyetamba kwenye kipindi cha vichekesho cha Vituko Show amesema kuwa wasanii wanatakiwa kubadilika kutokana na wao kuwa kioo cha jamii kwa hiyo siyo vizuri kwa wao kuiga mambo ya kigeni.

Mkongwe huyo wa sanaa nchini amesema kuwa vitendo hivyo vinachangia kushuka kwa kwa fani ya uigizaji nchini kutokana na kutofuatwa kwa maadili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *