Mzee Athuman Mchambua (76) ambaye ametoa tangazo la kutafuta mke wa kuoa, amesema anaamini atafanikiwa lengo lake kabla mwaka huu kumalizika.

Amesema hadi sasa ameshapokea simu za wanawake wa mikoa karibu yote ya Tanzania bara isipokuwa Pwani.

Mzee Mchambua amesema kuwa hatatumia tena njia ya kuweka madalali nchi nzima kama alivyoahidi awali, badala yake kuna mkakati mpya ambao anafikiria kuutumia utakaomrahisishia kukamilisha ndoto yake.

Mzee huyo amejipatia umaarufu ndani na nje ya nchi baada ya kuweka tangazo lenye sifa za mke anayemuhitaji mwezi mmoja uliopita kabla ya kuamua kulisitisha baada ya muda wake kumalizika.

Sifa kuu ambazo mzee huyo angependa mke anayemsaka awe nazo, ni pamoja na kuwa na usafi wa hali ya juu, mwenye kushika dini ya Kiislamu, uvumilivu wa ndoa, uwezo wa kilimo, upendo kwa mume, watoto na wajukuu.

Mzee Mchambua ana familia ya mke mmoja ambaye anaishi shamba, watoto 15 na wajukuu kadhaa.

Wiki iliyopita mzee huyo alitoa masharti mapya kwa mwanamke ambaye atabahatika kuolewa naye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *