Rais mstaafu wa awamu ya pili,  Ali Hassan Mwinyi leo amechangisha zaidi ya  Sh. 1.5b katika matembezi maalum yaliyofanyika kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi,  Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwachangia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10 mwaka huu.

Fedha hizo zimetokana na michango pamoja na ahadi za wadau mbalimbali waliojitokeza kushiriki kwenye matembezi hayo yaliyokuwa yakilenga kuchangia walioathirika na tetemeko na yaliitishwa na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa chini ya Waziri Dk Augustine Mahiga.

Matembezi hayo yalikuwa ni ya  kilometa tano. Akizungumza viwanjani hapo baada ya kukamilisha taratibu za uchangiaji wa fedha kwa ajili ya waathirika hao, Mwinyi aliwashukuru wote waliojitokeza na kuchangia zikiwemo taasisi mbalimbali na makampuni binafsi kwa kufanikisha zoezi hilo na kupatikana kiasi cha fedha hizo.

Hata hivyo amewataka kuendelea na moyo huo kila panapotokea maafa kwani alisema yatupasa kushikamana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *