Mwili  wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta umewasili jioni hii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ukitokea nchini  Ujerumani ambako alikuwa akitibiwa hadi mauti yalipomfika.

Mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege, mwili wa Marehemu Sitta umepelekwa nyumbani kwake Msasani, Dar es Salaam.

Kesho, Ijumaa saa tatu asubuhi kutakuwa na ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Sitta itakayofanyika katika Viwanja vya Karimjee ambako ndugu, jamaa, marafiki na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam watapata fursa ya kumuaga.

Baadaye mwili wa Sitta utasafirishwa hadi mkoani Dodoma ambako utaagwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kisha kusafirishwa kwenda Urambo mkoani Tabora kwa mazishi yatakayofanyika Jumamosi.

Marehemu Sitta alifariki dunia Novemba 07 mwaka huu katika Hospitali ya Technal University iliyopo nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya saratani ya tezi dume.

Picha kwa hisani ya Global Publishers

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *