Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameongoza mamia ya Watanzania kuuaga mwili wa aliyekuwa spika wa Bunge la Tanzania, Samweli Sitta mjini Dar es Salaam huku baadhi ya viongozi waliofanya naye kazi kuzungumza jinsi alivyokuwa spika huyo.

Mwili wa kiongozi huyo umeagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam huku pia wakiwepo marais wastaafu, mawaziri wa zamani na viongozi mbalimbali wa kisiasa nchini huku ndugu jamaa na marafiki.

Baada ya hapo mwili huo utaagwa katika ukumbi wa Bunge mkoani Dodoma kwa ajili ya wabunge kupata nafasi ya kumuaga spika wa bunge huyo mstaafu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *