Mwili wa Ndesamburo wawasili katika viwanja vya Majengo

0
321

Mwili wa aliyekuwa mbunge wa Moshi Mjini, Phillemon Ndesamburo umewasili katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya watu kutoa heshima zao za mwisho.

Ndesamburo ambaye alikuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro alifariki ghafla wiki iliyopita wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya KCMC iliyopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mwili wa Ndesamburo unatarajiwa kuagwa leo katika viwanja hivyo vya Majengo kabla ya kupelekwa kwake kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Viongozi wa juu wa Chadema pamoja na waasisi wa Chama hicho wapo katika viwanja hivyo kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho kwa kada huyo.

Viongozi wa Chadema waliohudhuria kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho ni Fredirck Sumaye, Edward Lowassa, Freeman Mbowe pamoja  muasisi wa chama hicho Edwin Mtei.

LEAVE A REPLY