Mwili wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum ( Chadema) marehemu Dkt. Elly Marko Macha unaagwa leo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanauaga mwili huo na baada ya hapo kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Arusha.

Marehemu Dkt. Elly Macha alikuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani.

Dkt Macha amefariki katika hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *