Aliyekuwa mume wa Zari The Bossy Lady, Ivan Ssemwanga anatarajiwa kuzikwa siku ya jumanne nyumbani kwao nchini Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na ndugu wa marehemu zinasema kuwa mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kesho siku ya Jumapili kutoka nchini Afrika Kusini kuelekea Uganda kwa mazishi.

Mjomba wa marehemu, Herbert Luyinda ameviambia vyombo vya habari nchini Uganda kwamba maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu yamekamilika na taratibu zote zinaenda vizuri.

Baada ya mwili wa marehemu kuwasili Uganda hapo kesho utafanyiwa ibada takatifu siku ya Jumatatu na siku ya Jumanne atazikwa kijijini kwao Nakaliro.

Ivan Don Ssemwanga ambaye ni mfanyabiashara maarufu Afrika Kusini alifariki dunia siku ya Alhamisi nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa maradhi ya shambulio la moyo.

Ivan ambaye alikuwa mume wa Zari amefanikiwa kuzaa watoto watatu ambao wote wa kiume.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *