Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, amesema kuwa milango ya uwekezaji nchini ipo wazi hivyo wawekezaji kutoka nje ya nchi wanakaribishwa kuwekeza katika fursa zilizopo.

Mwijage ameyasema hayo jana katika mkutano wa wafanyabiashara wa Tanzania na Ubelgiji uliofanyika jijini Dar es Salaam amesema mazingira yaliyopo ni bora kwa uwekezaji wa biashara kupitia Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC).

Waziri huyo amesema kuwa “Tanzania ni nchi inayokua kwa kasi duniani hivyo wawekezaji wana nafasi ya kufanya uwekezaji kutokana na kwamba hii ni nchi ya amani ambapo wanaweza kuwekeza na kuzalisha bila kuwepo kwa vikwazo,”.

Ameongeza kwamba miongoni mwa mambo yanayoweza kuwekezwa ni kilimo, usafirishaji, uboreshaji wa miundombinu ambapo alisema Mkoa wa Kigoma unazo fursa nyingi ikiwemo kilimo cha michikichi na miwa kwa kuzalisha sukari.

Pia amesema Tanzania na Ubelgiji zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu, hivyo milango ya uwekezaji ipo wazi kwa kuwekeza katika mradi wowote.

Picha kwa hisani ya Global Pushers

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *