Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ametolea ufafanuzi wa makaa ya mawe yanayozalishwa hapa nchini ikilinganishwa na yale yanayotoka nje ya nchi.
Mwijage amesema hilo linatokana na kuwa makaa hayo yanasafirishwa kwa barabara njia ambayo ni ya gharama kubwa tofauti na yale ya Afrika Kusini ambayo husafirishwa kwa njia ya majini ambayo ni gharama nafuu.
Pia amewataka wananchi kutambua kuwa serikali inathamini mchango wa kiwanda cha saruji cha Dangote ambacho amesema kimeongeza ushindani katika soko na kushuka kwa bei ya saruji na kuongeza kuwa nchi kwa sasa haiwezi kukumbwa na uhaba wa saruji.
Ufafanuzi huo unakuja kufuatia taarifa zilizoenea nchini kuwa kiwanda cha saruji cha Dangote kufungwa kutokana na gharama kuwa kubwa.