Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwingulu Nchemba amekabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya cha Ndago kilichopo wilayani Iramba mkoani Singida.

Gari hilo limetolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kituo hicho ili kutatua tatizo la ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa.

Wakati wa kukabidhi gari hilo waziri Nchemba amepiga marufuku wagonjwa kuombwa kuchangia mafuta ya ambulance hiyo au gharama yoyote ile na kuwataka wagonjwa kutumia gari hilo bure bila kuchajiwa gharama yeyote.

Mwigulu amesema kuwa Gari hilo lipatikane kituoni wakati wote, liwe na mafuta ya kutosha na dereva awepo. Gari hili ambalo ni la kisasa litunzwe na kulindwa ili liweze kutumika kwa miaka mingi ijayo.

Pia Mwigulu ameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli na waziri Ummy kwa msaada huo ambao utaokoa wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *