Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kati, Ikwiriri wilayani Rufiji, Athuman Mtoteka anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana akiwa  nyumbani kwake.

Mwenyekiti huyo ambaye anawakilisha chama cha Wananchi CUF, anadaiwa kutekwa jana kati ya saa moja na mbili usiku.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema  watu wasiojulikana walifika nyumbani kwake kwa miguu kisha kumchukua na  kwenda naye kusikojulikana.

Amesema taarifa za tukio hilo zilitolewa katika kituo cha Polisi Ikwiriri leo Alhamisi asubuhi na mkewe.
Lyanga ameeleza kuwa baada ya kutolewa kwa taarifa hizo kituoni hapo, Polisi tayari wamefungua jalada la uchunguzi dhidi ya tukio hilo.

Kadhalika taarifa toka kwa majirani wa mwenyekiti huyo zinaeleza kuwa waliwaona  watu watano waliofika nyumbani hapo wakitembea kwa miguu kisha kumkamata na kuondoka naye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *