Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi, Suleiman Mathew amehukumiwa na Mahakama ya Lindi kwenda jela miezi nane baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mkusanyiko bila ya kibali.

Mathew ambaye alikuwa mgombea ubunge katika jimbo la Mtama mkoani humo kupitia Chadema na kiongozi mwenzake wa kata wamehukumiwa kwenda jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mkusanyiko bila ya kibali.

Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Mkoa wa Lindi, mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mhina.

Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kujiridhisha kuwa ushahidi wao umethibitika bila kuacha shaka.

Waliotiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo ni Mwenyekiti Chadema mkoani Lindi, Selemani Methew pamoja na Katibu wa Tawi la Kata ya Nyangamala, Ismail Kupilila.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mhina alisema, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Juma Maige uliwafikisha mahakamani hapo mashahidi sita.

Amesema kutokana na ushahidi ulitolewa na mashahidi hao, mahakama imeona upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao bila kuacha shaka yoyote na kuwatia hatiani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *