Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha, Michael Lekule amemjia juu Edward Lowassa baada ya kusema kuwa Rais John Magufuli amemtuma ‘mtoto mdogo’ kwenda kuiwakilisha serikali kwenye mazishi ya wanafunzi wa  shule ya Lucky Vicent.

Lekule amesema kauli ya Lowassa ameitoa kwa kudanganya wananchi na kuonesha serikali ya Magufuli haishirikiani na wananchi .

Amesema jitihada za serikali ya Magufuli zimeonekana kupitia kwa wawakilishi wake Makamu wa Rais Samia Suluhu pamoja na Mrisho Gambo pamoja na wanachama wa CCM ambao walijitokeza kwa wingi kwenye msiba huo mzito

Pia alisema wamemshangaa kwa kusema Rais alimtuma mtoto mdogo wakati yeye mwaka 2007 ajali mbaya iliyotokea Monduli duka bovu na kuua watu 20 ambao 11 walikuwa ni askari wa JKT, Rais Kikwete alimtuma aje kuiwakilisha serikali.

Hata hivyo alimtaka kiongozi huyo, ajiulize kama yeye kipindi akiwa Waziri Mkuu aliweza kutumwa na Rais, amuwakilishe kwenye msiba wa watu 20, je yeye na Makamu wa Rais ni nani mdogo?.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *