Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Ubungo NHC, Amani Sizya amefunguka sababu za kufutwa kwa mtaa wa mchezaji wa Tottenham Vicent Wanyama.

Mwenyekiti huyo amesema ni kutokana na kutofuata taratibu wakati wa kutangazwa kwa mtaa huo.

“Kila jambo linautaratibu wake hata ukitaka kubadilisha jina la barabara lazima ufuate utaratibu kwahiyo hakukuwa na utaratibu uliofuatwa unajua ilikuwa haraka sana, lakini niseme tuu kwamba hili litafanikiwa na mtaa huo utatumika kwa jina hilo wakifuata taratibu,”.

Victor Wanyama wiki iliyopita alipewa mtaa ujulikanao kama Viwandani eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam ili rasmi uanze kutambulika kwa jina lake lakini jana Serikali ya mtaa huo iling’oa kibao cha maelekezo na kufuta mtaa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *