Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake rasmi leo katika mkoa wa Simiyu ambapo utapitia jumla ya miradi 43 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 8,450,841,622/=.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakati akitoa salamu za Mkoa huo kwa Kiongozi wa kitaifa wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 , Ndg.AmourHamad Amour  katika kijiji cha Bukundi wilaya ya Meatu ukitokea katika mkoa Singida.

Mtaka amesema kati ya fedha hizo shilingi 680,285,524 zinatokana na Nguvu za wananchi ,Serikali Kuu shilingi 4,524,439,388, Halmashauri Shilingi 352,000,875, Washirika wa Maendeleo Shilingi 635,559,935 na Sekta binafsi Shilingi 2,258,555,900/=

Amesema Mwenge wa Uhuru utafungua miradi 14, kuzindua 13, kutembelea na kuona miradi 16 katika sekta ya Elimu,Afya,Maji,Vijana na wanawake, Miundombinu ya barabara, Sekta ya Viwanda, Maliasili, Kilimo, Ushirika na Utawala bora.

Pia Mtaka amesema katika kutekeleza kwa vitendo ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu 2017 usemao “SHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YANCHI YETU”, Mkoa wa Simiyu umeweza kujipambanua katika utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja, Bidhaa Moja, Kiwanda Kimoja”.

Naye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru , NAmour Hamad Amour akifungua jengo la upasuaji kwa wanawake wajawazito katika kituo cha Afya Bukundi wilayani Meatu mbali na kuipongeza wilaya hiyo kwa kujali afya za wananchi wake hususani wanawake wajawazito pia alitaka mradi huo utunzwe na uthaminiwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *